Chama cha wamiliki wa Mabasi ya abiria TABOA umekanusha kuwa hakutakua na mgomo wa kusafirisha abiria hapo kesho kama ilivyoripotiwa 

Taharuki kubwa imezuka baada ya kusambaa kwa taaarifa ya Video ikitangaza mgomo wa nchi nzima kupinga Kanuni mpya za leseni.

Akizungumza Jijini Dsm Mwekahazina wa TABOA Issa Nkya amesema ni kweli wanapinga kanuni hiyo lakini hakuna mgomo bali kuna mgogoro wa kisheria na Sumatra.

Nkya amesema Jumatano ya November 15 kutakua na kikao na Sumatra kujadili kanuni na baada ya hapo tamko litatolewa.

Kwa upande Mkurugenzi wa huduma za Sheria kutoka Sumatra Tumaini Silaa amesema kanuni zinazolalamikiwa hazina tatizo lolote shida ni kwamba TABOA bado hawajizielewa.

Silaa amesema Kwenye mkutano wa Jumatano watawaelimisha wadau kuhusu kanuni hiyo, huku akitoa onyo kwa Mmiliki wa mabasi atakaethubutu kugoma.

Kanuni inayopigiwa kelele na TABOA ni ile inayosema kuwa dereva akifanya kosa, ataadhibiwa kwa kupelekwa Mahakamni na mmiliki wa basi hilo atatozwa faini.

Latest News

Amtumia ndugu yake kutoroka jela
14 Feb 2018 14:15 - Mohamed Mnzava

Mamlaka nchini Peru zimemkamata mfungwa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoroke jela kwa kumuacha ndugu yake pacha katika naf [ ... ]

Ukame Cape Town umekuwa 'Janga la kitaifa'
14 Feb 2018 14:05 - Mohamed Mnzava

Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town - mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji - kuwa janga  [ ... ]

Waziri Mwigulu azungumzia kampeni kuhusishwa na tukio la Mbunge Lissu
14 Feb 2018 13:51 - Mohamed Mnzava

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kesi ya kuumwa kwa Mbunge wa Singida [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.