Star Tv

Viongozi wa bodi katika vituo vya afya wilayani Tarime mkoani Mara wameonywa kuacha tabia ya kununua dawa za binadamu katika maduka ya nchi jirani ya Kenya badala yake watumie ya hapa nchini yaliyoidhinishwa na serikali.

Ni katika kikao cha kuunda bodi ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Tarime mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Apoo Tindwa anakemea viongozi wa bodi watakao kiuka agizo la serikali katika manunuzi ya dawa.

Nae mganga mkuu wa Hosipitali ya Halmashauri ya wilaya ya Tarime Hamidu Adinani alieza kwamba lengo la uundwaji wa bodi hizi za afya ni kuboresha huduma za afya kwa jamii.

Katika kikao hiki viongozi wa bodi za afya wametakiwa kuwa mstari wa mbele kujiunga na kuhimiza wananchi kujiunga na mifuko ya bima za afya ili kupunguza tatizo la kukosa matibabu katika vituo vya afya.

Picha na mtandao.

Latest News

Faida ya Kunywa Vikombe 3 vya kahawa kwa siku kiafya'
23 Nov 2017 09:28 - Mohamed Mnzava

Unywaji wa kahawa kiasi ni salama , na vikombe vitatu kwa siku vya kahawa vinaweza kuwa na faida kadhaa za kiafya , kuli [ ... ]

Raia wa Uingereza aliyeiomba mahakama imfunge''
23 Nov 2017 08:44 - Mohamed Mnzava

Baada ya kupigwa marufuku kuomba na kulala ovyo ovyo kwenye veranda za maduka katika mji wa Middlesbrough, Bradley Grime [ ... ]

Polisi wavamia wahamiaji Papua New Guinea
23 Nov 2017 08:26 - Mohamed Mnzava

Polisi wa Papua New Guinea (PNG) wameingia katika kituo cha mahabusu cha wahamiaji kilichokuwa kinamilikiwa na Australia [ ... ]

Other Articles

Social Media

Star Tv - Advertisement
Star Tv - Advertisement
Star Tv - Advertisement

Copyright © 2017 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.