KILIMO cha umwagiliaji kimetajwa kuwa mwarobaini wa tatizo la Uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira katika Bwawa la Mtera mkoani Iringa, ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imeshauriwa kuwekeza katika ujenzi wa miundiombinu ya umwagiliaji.

Kilimo cha umwagiliaji kimekuwa kikitajwa kuwa na tija kwa wakulima na hiyo ni kutokana na kilimo hiki kutokutegemea majira ya mvua, na wananchi wa Kata ya Izazi na Migori katika Tarafa ya Isimani Wilayani Iringa changamoto yao kuu ni namna ya upatikanaji wa mvua, ambapo himizo la kilimo hiki cha kutumia miundombinu wezeshi ya umwagiliaji kinatajwa kuchangia maendeleo kwa wananchi hawa ambao kwa kiwango kikubwa wanategemea shughuli za Uvuvi katika Bwawa la Mtera jambo linalotajwa kusababisha Uvuvi haramu.

Changamoto ya upungufu wa chakula ndiyo chanzo cha wananchi wengi kwa Izazi na Migori kulitegemea Bwawa la Mtera kwa shughuli za Uvuvi ili kujipatia Samaki na hata kusaidia kukuza uchumi kwa biashara hii ya Kitoweo cha Samaki, ambapo Robert Masunya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, amesema zipo mbinu zitakazosaidia kupunguza changamoto ya uharibifu wa mazingira katika maeneo yote kame likiwemo la Isimani.

Picha na mtandao.

Latest News

Amtumia ndugu yake kutoroka jela
14 Feb 2018 14:15 - Mohamed Mnzava

Mamlaka nchini Peru zimemkamata mfungwa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoroke jela kwa kumuacha ndugu yake pacha katika naf [ ... ]

Ukame Cape Town umekuwa 'Janga la kitaifa'
14 Feb 2018 14:05 - Mohamed Mnzava

Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town - mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji - kuwa janga  [ ... ]

Waziri Mwigulu azungumzia kampeni kuhusishwa na tukio la Mbunge Lissu
14 Feb 2018 13:51 - Mohamed Mnzava

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kesi ya kuumwa kwa Mbunge wa Singida [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.