Star Tv

Uelewa mdogo wa kina juu ya Elimu ya Ukimwi kati ya watu wazima na Vijana na Kuanza mahusiano ya Ngono katika umri mdogo kunatajwa kuwa ni sababu zinazochangia maambukizi Mapya kuwa makubwa kwa vijana Tanzania.

Hayo yamebainika katika warsha ya Wabunge wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ukimwi na tume ya kudhibi Ukimwi TACAIDS mjini Dodoma Mkurugenzi wa ufatiliaji wa Tathimini kutoka Tume hiyo Dr. Jerome Kamwela akabainisha hali ilivyo kwa sasa hapa nchini.

Mkurugenzi wa Tume hiyo Dr. Leonard Maboko akatolea ufanunuzi suala la mkanganyiko wa Takwimu Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ukimwi wakatoa mtazamo wao kuhusiana na juhudi zinazofanyika katika mapambano dhidi ya Ukimwi Waziri wan chi ofisi ya waziri mkuu Jenister Mhagama akawataka wajumbe kutumia vyema elimu watakayoipata.

Aidha Kiwango kidogo cha upimaji wa VVU kwa watoto waliozaliwa na akina mama wanaoishi na VVU Kunaelezwa kuwa ni moja kati ya changamoto katika kutekeleza Muitikio wa UKIMWI.

Picha na mtandao.

Latest News

Mzawa wa Zanzibar ashinda Turner Prize.
06 Dec 2017 08:51 - RobinLeah Madaha

Profesa Lubaina Himid ni mzaliwa wa Zanzibar ambaye ni mtanzania ametangazwa kuwa mshindi wa 'Turner Prize 2017'katika t [ ... ]

Carlifonia- Maelfu ya makazi yateketezwa .
06 Dec 2017 08:04 - RobinLeah Madaha

Karibu watu 27,000 walilazimishwa kukimbia manyumba yao usiku wa manane wakati moto mkubwa ulisamba kwa haraka kusini kw [ ... ]

Trump atambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
06 Dec 2017 07:47 - RobinLeah Madaha

Maafisa wa serikali ya Marekani wamesema kuwa rais Donald Trump, leo atautambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel [ ... ]

Other Articles

Social Media

Star Tv - Advertisement
Star Tv - Advertisement
Star Tv - Advertisement

Copyright © 2017 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.