Wanasayansi wamegundua kwamba nzi hubeba viini vingi vinavyosababisha magonjwa kuliko ilivyodhaniwa awali.

Nzi wa kawaida wanaopatikana nyumbani na nzi wanaopatikana sana kwenye mizoga huwa na bakteria zaidi ya aina 600, uchunguzi wa DNA umebaini.

Nzi hao huhusishwa na maradhi mengi ya binadamu ikiwa ni pamoja na magonjwa ya tumbo, sumu kwenye damu na nimonia.

Nzi hueneza bakteria kutoka eneo moja hadi jingine kwa kutumia miguu yao na madawa, utafiti umeonesha.Mtafiti Prof Donald Bryant wa chuo kikuu cha jimbo la Penn State anasema watu walikuwa wanafahamu kwamba nzi hueneza bakteria lakini hawkauwa wanafahamu vyema ni kwa kiasi gani.

Uchunguzi wa DNA ulitumiwa kuchunguza mkusanyiko wa bakteria waliopatikana katika nzi wa kawaida wa nyumbani (Musca domestica) na nzi wanaotegemea sana mizoga na vitu vinavyooza (Chrysomya megacephala).

Nzi wa kawaida wanaopatikana nyumbani, ambao hupatikana karibu kila eneo duniani waligunduliwa kuwa na aina 351 za bakteria.

Nzi hao wengine wenye kutegemea mizoga na vitu vilivyooza walikuwa na aina 316 za bakteria. Nzi hawa sana hupatikana katika mazingira yenye joto.

Bakteria wengi wanaweza kupatikana kwa pamoja katika nzi wote wawili."Hili linakufanya ufikirie sana unapoamua kununua mchanganyiko wa matunda njiani, ambayo yamekaa wazi kwa muda, ukiwa matembezini," amesema Prof Bryant.

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.