Karibu watu 27,000 walilazimishwa kukimbia manyumba yao usiku wa manane wakati moto mkubwa ulisamba kwa haraka kusini kwa jimbo la Carlifonia.

Watu wamehamishwa kwa lazima kutoka makwao katika miji ya Ventura na Santa Paula karibu kilomita 115 Kaskazini mwa Los Angeles.Wazima moto walionya kuwa moto huo ulikuwa unasambaa kwa haraka na hawangeweza kuuzima.

Ukichochewa na upepo mkali moto uliosambaa ukubwa wa maelfu ya ekari kwa saa chache.

Gavana wa California Jerry Brown ametangaza hali ya tahadhari katika kaunti ya Ventura akiihaidi kukukabili moto huo kwa vyoyote vile.Mapema iliripotiwa kuwa mtu mmoja alifariki kwenye ajali ya barabarani akijaribu kuukimbia moto huo, lakini idara ya wazima moto kaunti ya Ventura imesema kuwa hakuna mtu aliyepatikana kwenye gari hilo lilikuwa limepinduka.

Maafisa walisema kuwa mzima moto alijeruhiwa. Pia walisema kwa nyumba 150 zilikuwa zimeharibiwa na watu 260,000 walikuwa hawana umeme.

Kwa hisani ya BBC

Latest News

Amtumia ndugu yake kutoroka jela
14 Feb 2018 14:15 - Mohamed Mnzava

Mamlaka nchini Peru zimemkamata mfungwa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoroke jela kwa kumuacha ndugu yake pacha katika naf [ ... ]

Ukame Cape Town umekuwa 'Janga la kitaifa'
14 Feb 2018 14:05 - Mohamed Mnzava

Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town - mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji - kuwa janga  [ ... ]

Waziri Mwigulu azungumzia kampeni kuhusishwa na tukio la Mbunge Lissu
14 Feb 2018 13:51 - Mohamed Mnzava

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kesi ya kuumwa kwa Mbunge wa Singida [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.