Mfanyabiashara James Rugemalila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anahitaji kuonana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ili ampe ushahidi wa nani anayepaswa kukamatwa katika kesi hiyo.

December 8, 2017 Rugemarila aliieleza mahakama hiyo kuwa unahitajika ushirikiano baina yake na upande wa mashtaka ili kumbaini mwizi wa Sh.Bil 309 za Serikali.

Mbali ya Rugemarila, Mshtakiwa mwingine ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309.

Rugemarila ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai kudai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba ahirisho.

Baada ya kueleza hayo, Rugemarila alinyoosha mkono ambapo amesema kuwa anaushukuru upande wa mashtaka ulimchukua gerezani na kumpeleka Upanga kwa mahojiano na kumrudisha salama gerezani.

“Leo nimekuja na ushahidi, hivyo naomba nikutane na DPP ili niweze kumsaidia kumjua mwizi anayepaswa kukamatwa, kwani lengo letu ni kuonyesha kuwa tupo Innocent,” alieleza Rugemarila.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Shaidi alimtaka Rugemarila kuwasiliana na mawakili wake ili waandike barua ya kuwasilisha kwa DPP kuhusu suala hilo la ushahidi wake, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi January 5, 2018.

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.