Watu zaidi ya 37 wamefariki baada ya mafuriko na maporomoko ya ardhi kuukumba mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa kufuatia mvua kubwa.

Wengi wa waliouawa ni wakazi wa mitaa ya mabanda ambapo nyumba nyingi zimeharibiwa na maji ya mafuriko na maporomo ya ardhi. Wengi kati ya wakazi milioni kumi wa mji wa Kinshasa huishi katika makazi duni katika maeneo tambarare na miundo mbinu ya kuondoa maji taka ni duni.

Waziri wa jimbo anayeangazia masuala ya kiafya na kijamii Dominique Weloli, alisema wengi wa waliofariki ambao ni pamoja na "watoto wawili au watatu waliokufa maji" walikuwa wanaishi Ngaliema, mtaa duni ambao umeathirika sana.

Kumekuwa na matukio ya vifo vinavyotokana na mafuriko karibu kila mwaka msimu wa mvua kubwa.

Kwa hisani ya BBC

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.