Naibu Spika Tulia Ackson amewaongoza waombolezaji Jijini Dar Es Salaam katika kuuaga mwili wa Mke wa Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kangi Lugola, ACP Mary Lugola .

Vilio na simanzi vilitatawala nyumbani kwa Naibu waziri kangi Lugola mara baada ya kuanza kwa zoezi la kuuaga mwili wa marehemu.

Ndipo ukafika wakati wa kiongozi wa Bunge kuongea katika msiba huo naibu Spika Dkt Tulia Ackson kwa niaba ya Bunge la Tanzania akasema mwenyezi Mungu umuita Mtu wake wakati wowote hivyo ni vyema tukatenda mema wakati wote.

Kwa huzuni kubwa mume wa marehemu Kangi Lugola akasimama nakuongea mbele ya waombolezaji akiwakumbusha binadamu kutojisahau kwa kupanga mipango binafsi kumbe mpangaji wa yote ni Mwenyezi Mungu.

Hatimaye Jeshi la polisi pamoja na Chama cha Mapinduzi kupitia wawakilishi wao wakatoa salamu za rambirambi.

Marehemu Mary Lugola Mpaka anafariki Dunia alikua ni Afisa Mnadhimu Polisi Reli amefariki tarehe 1 mwezi Januari kwa niaba ya familia alikua akisumbuliwa na shinikizo la damu,mwili wake umesafirishwa kutoka Jijiji Dar es salaam kwenda Mwibala wilayani Bunda Mkoani Mara kwa ajili ya Mazishi.

Picha na mtandao.

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.