Mgodi wa ACACIA umesaini mkataba na Halmashauri ya Msalala na Nyangh’wale kuanza mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria utakaogharimu shilingi bilioni 4.5 na kunufaisha vijiji 14.

Wakizungumza katika Siku ya Familia iliyoandaliwa na Mgodi huo Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu amesema tatizo la Maji ni Changamoto ya nchi nzima na mradi huu utasaidia kwa kiasi kikubwa.

Mradi huo unasimamiwa na Mwauwasa utawanufaisha wakazi laki na nusu

Miradi ambayo Mgodi iliahidi kufanya kabla ya kupunguza uzalishaji itaendelea kama kawaida.

Miradi mingine mikubwa inayotekelezwa na Acacia baadhi yake ni ujenzi wa majengo awamu ya pili kukamilisha Hospitali ya Bugarama uliogharimu bilioni 1.1 na milioni 200 zimetumika kujenga uzio katika Shule ya Msingi Kakola A na B.

Picha na mtandao.

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.