Liverpool inajiandaa kwa jaribio la pili kumsajili kiungo wa wakti wa Monaco mwenye umri wa miaka 22 Thomas Lemar wa Ufaransa baada ya kukataa kandarasi mpya katika klabu hiyo ya ligi ya daraja la kwanza. Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola hatoanzisha tena harakati za kutaka kumsajili winga wa Leicester raia wa Algeria mwenye umri wa miaka 26 Riyad Mahrez mwishoni mwa msimu huu. (mirror) Mkufunzi wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ambaye anahusishwa na kuchukua mahala pake Antonio Conte wa Chelsea anajiandaa kuelekea nchini Uingereza. Hatahivyo mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 47 hataki kumrithi Conte hadi mwisho wa msimu huu. Tottenham inataka kumsaini kiungo wa kati wa Watford na Ufaransa Abdoulaye Doucoure mwishoni mwa msimu huu Beki wa Brazil Fabinho mwenye umri wa miaka 24 ambaye klabu ya Manchester United ilikuwa inamnyatia msimu uliopita anasema kuwa muda wake katika klabu ya Monaco unakamilika(Metro) Klabu ya ligu kuu nchini China Hebei China Fortune inajiandaa kuwasilisha ombi jingine kwa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 30, baada ya ombi lao la kwanza kukataliwa. (Mundo Deportivo - in Spanish) Kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk Fred amechagua klabu ya Manchester City kama klabu anayopanga kuhamia , kulingana na mkufunzi wa zamani Mircea Lucescu. Raia huyo wa Brazil mwenye umri wa 24 pia amehusishwa na majirani wa City Manchester United. (Mirror) Kwa hisani ya BBC

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.