Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetoa ripoti inayoeleza kupungua kwa kesi za mimba katika umri mdogo duniani kote.

Shirika hilo limeeleza kuwa takriban ndoa za utotoni Milioni 25 zimezuiwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ambapo kwa sasa mtoto mmoja kati ya watano wanaolewa kabla ya umri wa miaka 18 ukilinganisha na mmoja kati ya wanne aliyekuwa anaolewa kipindi hicho. Nchi za kusini mwa Bara la Asia pia zimepunguza ndoa za utotoni huku Afrika ikiendelea pia kujitahidi kukabiliana na tatizo hilo ambapo kwa nchi kama Ethiopia imepunguza tatizo hilo kwa theluthi. Ripoti hiyo inaeleza kuwa mzigo wa ndoa za utotoni unaendelea kuzilemea nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambako jitihada zaidi zinahitajika ili kuondoa tatizo hilo kabisa. UNICEF inasema kuwa mmoja kati ya watoto watatu wanapitia ndoa za utotoni kwa kipindi hiki Afrika ukilinganisha na mmoja kati ya watoto watano waliokuwa wakiolewa miaka kumi iliyopita. Viongozi wa dunia wameapa kumaliza tatizo la ndoa za utotoni ifikapo mwaka 2030 chini ya Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs).

Latest News

Trump akubali mualiko wa kukutana na Kim Jong Un
09 Mar 2018 12:20 - Mohamed Mnzava

Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani  [ ... ]

Wanawake DRC wanapigania haki zao kumiliki ardhi
09 Mar 2018 12:15 - Mohamed Mnzava

Wanawake wanaoishi vijijini huko Jamhumuri ya Kidemokrasi ya Kongo, hawana haki ya urithi wa mali pamoja na ardhi iliyoa [ ... ]

Rais Kenyatta, Odinga wakutana, waapa kufanya kazi pamoja
09 Mar 2018 11:15 - Mohamed Mnzava

Kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya uliofanyika October 2017, na kuleta mkanganyiko mkubwa wa kisias [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.