Klabu ya Azam FC imeachana na mshambuliaji wake Yahaya Mohammed raia wa Ghana baada ya kushindwa kufanya vizuri kufuatia makubaliano ya pande zote mbili.

Yahaya alikuwa na mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo lakini kutokana na kushindwa kutimiza vizuri majukumu yake jana uongozi ulikaa na mchezaji huyo kabla ya kufikia maamuzi yakuachana nae.

Msemaji wa klabu huyo Jaffer Idd amesema baada ya kuondoka kwa mchezaji huyo uongozi unatafuta mbadala wake ambaye anaweza kutoka ndani au nje ya nchi.

"Ni rasmi kuanzia jana tuliachana mchezaji wetu Yahaya Mohammed baada ya makubaliano ya pande zote na leo
ataondoka kuelekea kwao Ghana," alisema Jaffer.

Jaffer amesema mchezaji huyo amepewa barua yake na wamemtakia kila la kheri katika maisha yake ya mapya ya soka.

Mchezaji huyo alichangia kwa kiasi kikubwa ubingwa wa michuano ya Mapinduzi iliyofanyika visiwani Zanzibar mwaka huu huku pia akiwa ndiye aliyefunga bao la kwanza la Azam msimu huu.

Latest News

Amtumia ndugu yake kutoroka jela
14 Feb 2018 14:15 - Mohamed Mnzava

Mamlaka nchini Peru zimemkamata mfungwa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoroke jela kwa kumuacha ndugu yake pacha katika naf [ ... ]

Ukame Cape Town umekuwa 'Janga la kitaifa'
14 Feb 2018 14:05 - Mohamed Mnzava

Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town - mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji - kuwa janga  [ ... ]

Waziri Mwigulu azungumzia kampeni kuhusishwa na tukio la Mbunge Lissu
14 Feb 2018 13:51 - Mohamed Mnzava

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kesi ya kuumwa kwa Mbunge wa Singida [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.