Nyota wa filamu Portia de Rossi amemtuhumu nyota mwenza wa filamu na mtayarishaji Steven Seagal kwa unyanyasaji wa kinjinsia.

Nyota huyo wa filamu ya The Arrested Development , ambaye ameolewa na mtangazaji wa Marekani Ellen DeGeneres, alitoa madai hayo katika chapisho la ujumbe wa Twitter siku ya Jumatano usiku.

Anadai wakati wa ukaguzi wa kuwaajiri wale watakaoigiza katika filamu, bwana Seagl alimwambia umuhimu wa wao wawili kulala pamoja kabla ya kufungua zipu ya suruali ndefu aliyokuwa amevaa.Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 65 anajulikana kwa uigizaji wake miaka 1980 na 1990, ikiwemo filamu ya Under Siege na Flight of Fury.

Alipewa uraia wa Urusi na rais wa taifa hilo Vladmir Putin 2016.

Wanawake wengine kadhaa wamejitokeza kumshutumu bwana Seagal kwa kuwa na tabia mbaya akiwemo nyota wa filamu ya Good Wife Julianna Margulies na mwanamitindo Jenny McCarthy.

Latest News

Amtumia ndugu yake kutoroka jela
14 Feb 2018 14:15 - Mohamed Mnzava

Mamlaka nchini Peru zimemkamata mfungwa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoroke jela kwa kumuacha ndugu yake pacha katika naf [ ... ]

Ukame Cape Town umekuwa 'Janga la kitaifa'
14 Feb 2018 14:05 - Mohamed Mnzava

Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town - mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji - kuwa janga  [ ... ]

Waziri Mwigulu azungumzia kampeni kuhusishwa na tukio la Mbunge Lissu
14 Feb 2018 13:51 - Mohamed Mnzava

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kesi ya kuumwa kwa Mbunge wa Singida [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.