Star Tv

Rais Donald Trump amemwambia waziri mkuu wa Uingereza Theresa May kuangazia ugaidi nchini Uingereza badala ya kumkosoa kwa kusambaza video za kundi la mrengo wa kulia la Uingereza ambalo linaeneza chuki.

''Usiniangazie sana mimi, angazia ugaidi unaotekelezwa na makundi yalio na itikadi kali ambao unatekelezwa nchini humo'', Trump alituma ujumbe wa Twitter.

Rais huyo wa Marekani awali alituma video tatu zenye chuki zilizosambazwa katika mtandao wa Twitter na makundi hayo nchini Uingereza.

Msemaji wa bi May alisema kuwa ni makosa kwa rais kufanya hivyo.

Marekani na Uingereza ni washirika wa karibu na wameelezewa kuwa na ''uhusiano maalum''.

Theresa May alikuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kumtembelea rais Trump katika ikulu ya Whitehouse.

Kanda za video zilizosambazwa na Trump ambaye ana takriban wafuasi milioni 40 awali zilikuwa zimechapishwa na Jayda Fransen, naibu kiobngozi wa kundi la Uingereza la Britain First, kundi lililoanzishwa na wanachama wa zamani wa mrengo wa kulia wa chama cha Uingereza cha BNP.

Bi Fransen mwenye umri wa miaka 31 ameshtakiwa nchini Uingereza mwa kutumia maneno ya kutisha, na matusi katika hotuba alizotoa katika mkutano mjini Belfast.

Wanasiasa nchini Uingereza wameukosoa ujumbe huo wa rais Trump akiwemo, askofu mkuu wa Cantebury Justin Welby ambaye alisema kuwa inakera kwamba rais Trump aliamua kulipatia sauti kundi lenye itikadi kali la mrengo wa kulia.

Hatua hiyo imezua hisia kali huku baadhi ya raia wakitaka ziara ya rais Trump nchini Uingereza kufutiliwa mbali ,ijapokuwa afisi ya waziri mkuu imesema kuwa ziara hiyo bado itafanyika.

Latest News

Mzawa wa Zanzibar ashinda Turner Prize.
06 Dec 2017 08:51 - RobinLeah Madaha

Profesa Lubaina Himid ni mzaliwa wa Zanzibar ambaye ni mtanzania ametangazwa kuwa mshindi wa 'Turner Prize 2017'katika t [ ... ]

Carlifonia- Maelfu ya makazi yateketezwa .
06 Dec 2017 08:04 - RobinLeah Madaha

Karibu watu 27,000 walilazimishwa kukimbia manyumba yao usiku wa manane wakati moto mkubwa ulisamba kwa haraka kusini kw [ ... ]

Trump atambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
06 Dec 2017 07:47 - RobinLeah Madaha

Maafisa wa serikali ya Marekani wamesema kuwa rais Donald Trump, leo atautambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel [ ... ]

Other Articles

Social Media

Star Tv - Advertisement
Star Tv - Advertisement
Star Tv - Advertisement

Copyright © 2017 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.