Star Tv

Uingereza na Muungano wa Ulaya zimefikia mkataba wa baada ya Brexit kumaliza mvutano wa miezi kadhaa kuhusu kanuni za biashara na haki ya uvuvi.

Katika mzungumzo na wanahabari Downing Street, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema: "Tumechukua tena udhibiti wa sheria zetu na hatima yetu."

Bw. Johnson ameongeza kuwa japo mashauriano yalikuwa "makali" ulikuwa "mkataba mzuri kwa Ulaya nzima", utakaobuni nafasi za kazi na ustawi.

Mkuu wa Muungano wa Ulaya (EU) Ursula von der Leyen amesema mkataba huo ulikuwa wa "haki na usawa".

Aliongeza kuwa,  "sasa ni wakati wa kuangazia hatua inayofuata" na kuongeza kuwa Uingereza "itasalia kuwa mshirika wa kuaminika", na kutakuwa na kipindi cha miaka tano na nusu cha kwa sekta ya uvuvi, alisema.

Imebainishwa kuwa ushirikiano utaendelea kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabia ya nchi, usalama na usafiri.

Waziri Mkuu Boris amepongeza namna mkataba huo ulivyofikiwa kati ya Uingereza na EU.

Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, Waziri Mkuu huyo alisema; "Tumekamilisha mpango mkubwa zaidi utakaogharimu pauni bilioni 668 kwa mwaka".

Mkataba kamili wa mitindo ya Canada umefikiwa kati ya Uingereza na EU, Mkataba ambao utalinda ajira kote nchini.

Pia utawezesha bidhaa za Uingereza kuuzwa bila ushuru, bila upendeleo katika soko la EU.

Amesema anatumai Bunge la Uingereza litarejelea vikao vyake mnamo 30 Desemba kupiga kura juu ya mpango huo, pia itahitaji kupitishwa na Bunge la Ulaya.

Chama cha Upinzani cha Labour ambacho kinatarajiwa sana kuunga mkono makubaliano hayo kimesema kitatoa kauli yake rasmi "kwa wakati unaofaa".

Mpango huo umewapa afueni kubwa kwa wafanyabiashara wengi wa Uingereza, ambao tayari wanaathirika kutokana na athari za janga la corona.

Huku wakihofia usumbufu katika mipaka wakati Uingereza itakapojiondoa katika sheria za biashara za EU Alhamisi ijayo.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.