Star Tv

Idadi ya wajumbe wa Republican imeongezeka, wakiungana na juhudi za Rais Donald Trump kupinga matokeo ya uchaguzi wa Marekani uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2020.

Maseneta hao wamesema wanayakataa matokeo ya uchaguzi huo wakati Bunge litakapoandaa kikao wiki ijayo cha kuhesabu kura za wajumbe maalum maarufu kama Electoral College na kuidhinisha ushindi wa Rais mteule Joe Biden.

Seneta Ted Cruz wa jimbo la Texas ametangaza muungano wa maseneta 11 na maseneta wateule ambao wamedhamiria kuyapinga matokeo hayo katika kikao cha pamoja cha mabaraza yote mawili ya bunge Jumatano ijayo.

Kiongozi wa Warepublican katika Seneti Mitch McConell alikiomba chama chake kutojaribu kukibatilisha kile ambacho maafisa wasioegemea chama chochote wamesema ni uchaguzi uliokuwa wa huru na haki.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.