Star Tv

Rais wa John Pombe Magufuli amempongeza mwanasiasa wa upinzani Maalim Seif Shariff kwa kukubali kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) visiwani Zanzibar.

Rais Magufuli amesema kuwa uamuzi huo wa Maalim Seif ulikuwa ni wa busara na ulioangalia maslahi ya Zanzibar.

"Uliacha maslahi yako binafsi, ukafanya uamuzi mkubwa na wa busara kwa maslahi ya Wazanzibari," ameeleza Magufuli na kuongeza: "Kuna ndoa zilivunjika, hasa Pemba kutokana na uchaguzi kwa kuwa mwanamke kapigia kura CCM na mume ACT, lakini baada ya maamuzi ya Maalim Seif wanandoa hao wakarudiana."-Rais Magufuli.

Mwezi Desemba ACT ilitangaza kukubali kuingia katika serikali ya Zanzibar kama katiba ya visiwa hivyo inavyoelekeza na kupendekeza jina la Maalim Seif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Maamuzi ambayo yalipokelewa kwa hisia mseto huku baadhi ya wanaharakati wakikikosoa chama hicho kwa 'kuwasaliti wananchi.

Rais Mwinyi na Maalim Seif wapo nyumbani kwa rais Magufuli wilayani Chato kwa ziara ya siku mbili.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.