Star Tv

Mgombea wa urais nchini Uganda, Bobi Wine amepinga matokeo ya uchaguzi ambayo yametangazwa hadi sasa na kujitaja binafsi kama rais mteule, licha ya tume ya uchaguzi kusema kuwa sio kura zote zilizokwisha hesabiwa.

Bobi Wine anadai uchaguzi wa Alhamisi ulitawaliwa na wizi mbaya zaidi wa kura kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Uganda, lakini hakutoa ushahidi wowote kuhusu madai yake.

Matokeo ya awali yanayotolewa na Tume ya uchaguzi yanaonesha Rais Yoweri Museveni anaongoza kwa zaidi ya 60%.

Bobi Wine amewaambia waandishi wa habari kuwa anaamini intaneti na mitandao ya kijamii vilifungwa ili kama njia ya kuvuruga kura.

Mgombea wa upinzani tayari amedai kuwa kulikuwa na wizi na mawakala wake pamoja na wawaikilishi wameendelea kukamatwa.

Lakini mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi, Simon Byabakama, amesema kuwa Bobi Wine ana jukumu la kutoa ushahidi kwamba kuna wizi.

Amesema kuwa wagombea walikuwa na mawakala ambao walishuhudia kuhesabiwa kwa kura katika vituo vya kukusanya na kuhesabu kura.

Ni vituo viwili tu vya upigaji kura vilivyoripoti dosari na shughuli ya kupiga kura ikasitishwa katika vituo hivyo, Na katika kituo kimoja cha kupigia kura, mtu mmoja alitoroka na sanduku la kura.

Chanzo na BBC Swahili.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.