Star Tv

Yoweri Museveni ametangazwa kuwa rais mteule wa Uganda baada ya kupata ushindi wa kura asilimia 58.64.

Tume ya Uchaguzi Uganda (EC) imemtangaza Yoweri Kaguta Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Alhamisi tarehe 14 Januari 2021.

Kwa mujibu wa EC Bw Museveni amepata kura 5,851,037 sawa na asilimia 58.64 ya kura zote zilizopigwa.

Mpinzani mkuu wa Museveni, mwanamuziki Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 3,475,398 sawa na asilimia 34.83 ya kura zote.

Bobi Wine hata hivyo alitangaza kutokukubaliana na matokeo hapo jana wakati tume ya EC ilipokuwa ikiendelea kutangaza matokeo.

Idadi kamili ya watu waliopiga kura ni 9,978,093 ikiwa ni sawa na asilimia 57.22 tu ya idadi ya watu waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

Rais Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 35 akiwa atakuwa anaingia kuongoza kwa muhula wa sita.

Bwana Museveni mwenye miaka 76-anasema kuwa amelifanya taifa hilo kuwa na maendeleo wakati Bobi Wine, ambaye ana miaka 38, jina lake halisi likiwa Robert Kyagulanyi, anasema anawakilisha vijana ambapo Uganda likiwa ni taifa ambalo lina vijana wengi zaidi duniani.

Ijumaa, wakati matokeo yakianza kutangazwa bwana Wine alisema askari walikuwa wameizingira nyumba yake, Lakini msemaji wa serikali alimshutumu kwa kuweka taharuki isiyo na ukweli ili kupata huruma ya watu.

Aidha, Wakati pia Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikiyatangaza matokeo hayo Jumamosi mchana, makazi ya Bobi Wine yaliyoko nje kidogo ya mji mkuu, Kampala bado yalikuwa yamezingirwa na wanajeshi.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.