Star Tv

Rais mteule wa Marekani Joe Biden atatia saini maagizo 12 ya rais siku ya kuapishwa kwake kuwa rais wiki ijayo ili kushughulikia janga la virusi vya corona, uchumi wa nchi hiyo unaodorora, mabadiliko ya hali ya hewa na ubaguzi wa rangi.

Haya ni kwa mujibu wa mkuu wa utumishi anayetarajiwa Ron Klain katika taarifa aliyoitoa jana Jumamosi.

Klain amesema kuwa mizozo yote hii inahitaji kushughulikiwa kwa haraka na kuongeza kuwa Biden atatia saini takriban maagizo 12 ya rais baada ya kuapishwa siku ya Jumatano.

Klain aliongeza kuwa katika siku zake 10 za kwanza ofisini, Biden atachukua hatua madhubuti kushughulikia mizozo hiyo minne, kuzuia madhara mengine ya haraka na yasiyoweza kurekebishwa, na kurudisha nafasi ya Marekani ulimwenguni.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.