Star Tv

Rais mteule wa Marekani Joe Biden aliwasili Washington katika mkesha wa sherehe ya kuapishwa kwake, wakati mtangulizi wake Donald Trump ambaye atasusia hafla hiyo ya kula kiapo kwa mara ya kwanza akiitakia mafanikio serikali mpya.

Machozi yalimtoka Biden katika sherehe ya kuagwa mjini Wilmington, Delaware, ambako alitoa heshima kwa marehemu mwanawe wa kiume kabla ya kupanda ndege kuelekea katika mji mkuu.

Kwa upande wake, Trump ambaye hajaonekana hadharani kwa wiki moja sasa, alivunja ukimya wake wa siku nyingi kupitia hotuba iliyorikodiwa kwenye mkanda wa video.

Trump kwa mara ya kwanza aliiwaomba Wamarekani ''kuiombea'' mafanikio serikali ijayo ya Biden, ikiwa ni mabadiliko ya msimamo wa wiki nyingi alizotumia kuishawishi idadi kubwa ya wafuasi wake wa Republican kuwa Biden alifanya udanganyifu katika kinyang’yiro cha urais.

Chanzo na DW.

 

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.