Star Tv

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ameitaka Bodi ya mfuko wa Barabara (RfB) kutumia vifungu vya sheria vitakavyowabana watumiaji wa barabara wanaoegesha magari kwenye mabega ya barabara, wanaoiba alama za barabarani pamoja na wanaopitisha mifugo kwenye barabara.

Mhandisi Kasekenya ameyasema hayo, alipotembelea ofisi za Mfuko huo zilizoko Njedengwa, jijini Dodoma ili kujifunza shughuli zinazofanywa na mfuko huo.

“Simamieni sheria na muwachukulie hatua wale wote wanaohujumu miundombinu ya barabara kwa namna moja ama nyingine ili tuzilinde barabara zetu na kutotumia fedha nyingi katika matengenezo”. amesema Mhandisi Kasekenya.

Aidha, amewataka Mameneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanaziba mashimo barabarani ndani ya masaa 48 kama sheria inavyoelekeza ili kupunguza ajali zinazoweza kutokea kutokana na uwepo wa mashimo hayo.

Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Eliud Nyauhenga, pamoja na mambo mengine amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa Mfuko unafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kukusanya fedha, kugawa fedha kwa Taasisi husika pamoja na kufuatilia matumizi ya fedha hizo.

Nyauhenga amebainisha kuwa asilimia 70 ya makusanyo inapelekwa kwenye ukarabati wa barabara za kitaifa ambazo ziko chini ya wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na asilimia 30 inapelekwa kwenye ukarabati wa barabara zilizoko chini ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

Naibu Waziri Kasekenya, ametembelea Bodi ya Mfuko wa Barabara ambayo imekuwa ikitoa fedha kwa ajii ya matengenezo ya barabara nchini zinazosimamiwa na TANROADS pamoja na TARURA na kuhakikisha kuwa hali ya mtandao wa barabara nchini inakuwa bora.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.