Star Tv

Mkuu  wa  wilaya  ya  Kalambo Julieth Binyura  amemweka ndani  kwa muda  wa  saa 24 mtendaji  wa  kijiji cha  Mau kata ya Mbulima John Ndasi baada ya kuzitafutana fedha za vitambulisho vya wajasiliamali kiasi cha shilingi milioni moja na elfu themanini.

Kumekwepo na changamoto ya baadhi ya watendaji  kuto rejesha  fedha za vitambulisho  vya ujasilimali licha  ya kutoa  vitambulisho  kwa wafanyabishara na kupatiwa fedha  na hivyo kupelekea uongozi wa  wilaya  hiyo  kuanzisha  oparesheni  ya  ukaguzi wa vitambulisho hivyo kupitia  kwa  watendaji  na kubaini  baadhi  ya  watendaji  kula fedha hizo kinyume  na utaratibu.

Akiongea  kwa  niaba ya mkuu wa wilaya  hiyo katibu  tawala wilayani  humo Frank Schalwe, amesema wamelazimika  kuchukua hatua  ya  kumweka  ndani  mtendaji  wa kijiji cha Mau baada ya kula fedha  za  vitambulisho kiasi cha shilingi million moja na elfu themani.

Mkurugezi  mtendaji wa halmashauri hiyo Msongela Palela amewaonya watendaji kuacha tabia ya kuzitumia  fedha  za vitambulisho  katika  matumizi   yao  binafus  na  kusema  atakae  bainika  hatua kali za kishera  dhidi  yake  zitachukuliwa.

Aidha  Msongera  amewataka  watendaji  kuwa  wabunifu husunai  wakati  wa ukusanyaji  wa  fedha  hizo  kwa  lengo  la  kuondokana na matatizo  yasio kuwa  ya lazima.

Hata  hivyo  serikali  ilitoa  vitambulisho elfu , 13250mia mbili hamsini  na  huku  mpaka sasa vitambulisho 3065 vikiwa  vimetolewa  kwa  wafanyabiashara.

Latest News

Kumbukumbu ya miaka 20 ya Hayati Mwalimu Nyerere
14 Oct 2019 12:52 - Kisali Shombe

Kila tarehe 14/10 Tanzania inaazimisha kumbukumbu ya kifo cha hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwa [ ... ]

Mgogoro machimbo ya Shilalo Mwanza: Serikali yasitisha uchimbaji wa Dhahabu
11 Oct 2019 10:14 - Grace Melleor

Serikali imesitisha kwa muda usiojulikana shughuli za uchimbaji wa Madini ya Dhahabu katika machimbo ya Shilalo wilayani [ ... ]

Kesi Ya Uhujumu Uchumi: Sethi Na Rugemalira Waandika Kuomba Msamaha
11 Oct 2019 09:46 - Grace Melleor

Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imeeelezwa, Seth aliandika barua yake iliyopitia kwa Mkuu [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.