Star Tv

Halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara imetenga zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano ili kuwapa wakulima mbegu ili kunusuru zao la Alizeti kutokana na kiwanda cha kuongeza thamani ya zao hilo kukosa malighafi.

Serikali imewataka wawekezaji kuwekeza kwenye viwanda nchini ili viweze kuongeza  thamani ya mazao toka mashambani. Kiwanda cha kuchenjulia mafuta ya Alizeti cha Mossegi kilichopo wilayani Serengeti mkoani Mara kinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa malighafi hatua inayoelezwa kuwatia hasara wawekezaji. Pamoja na tatizo hilo lakini pia kiwanda hicho kinatatizo la kukatika umeme mara kwa mara suala linalofanya  gharama za uendeshaji kuwa juu katika uendeshaji wake.

Kutokana na hali hiyo halmashauri ya wilaya ya Serengeti imetenga fedha zaidi ya shilling miilioni ishirini na tano ili kuweza kunusuru hali hiyo kwa kuwagawia mbegu wakulima.

 

 

Latest News

Kumbukumbu ya miaka 20 ya Hayati Mwalimu Nyerere
14 Oct 2019 12:52 - Kisali Shombe

Kila tarehe 14/10 Tanzania inaazimisha kumbukumbu ya kifo cha hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwa [ ... ]

Mgogoro machimbo ya Shilalo Mwanza: Serikali yasitisha uchimbaji wa Dhahabu
11 Oct 2019 10:14 - Grace Melleor

Serikali imesitisha kwa muda usiojulikana shughuli za uchimbaji wa Madini ya Dhahabu katika machimbo ya Shilalo wilayani [ ... ]

Kesi Ya Uhujumu Uchumi: Sethi Na Rugemalira Waandika Kuomba Msamaha
11 Oct 2019 09:46 - Grace Melleor

Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imeeelezwa, Seth aliandika barua yake iliyopitia kwa Mkuu [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.