Star Tv

Mahakama ya hakimu mkazi Tarime mkoani Mara imewahukumu kifungo cha miaka 18 jela ama kulipa faini ya shilling million 315 raia kutoka nchini China kwa kukutwa na viroba tisa vyenye mchanga na boksi moja la madini wakisafirisha katika gari namba KBW 515  Toyota land Cruiser.

Kufuatia mkurugenzi wa mashitaka nchini DPP kutoa kibali cha kusikiliza kesi ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi na kukutwa na madini kinyume cha sheria Raia watatu wa China. Mahakama ya hakimu mkazi Tarime mkoani Mara imewatia hatiani watu hao watatu  kwa makosa mawili kila mmoja na kuwahukumu kifungo cha miaka 18 ama kulipa faini ya shilling  millioni mia tatu kumi na tano za Kitanzania huku gari walilokuwa nalo aina ya lend Cruiser namb KBW 515 L likitaifishwa.

Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama hiyo mheshimiwa Veronica Mgendi amesema kuwa washitakiwa hao watatu kwa pamoja  walitenda makosa hayo kinyume cha sheria za nchini hivyo adhabu hiyo liwe fundisho. Awali wanasheria wa serikali wametoa maelezo ya shitaka hilo mbele ya mahakama hiyo wakisema kuwa washitakiwa hao watatu kwa pamoja wilayani Tarime walikuwa  na gari ambalo limesheheni mali hiyo kinyume cha sheria. Mnamo tarehe 12/6/2019 raia hao  walikamatwa Nkenge wilayani Tarime wakiwa na mchanga kilo 3.75 wa madini ya aina mbali mbali wakiyasafirisha bila kibali.

Latest News

WATU WATANO WAFARIKI BAADA 'KUSHIKWA MATEKA' KANISANI.
11 Jul 2020 16:57 - Grace Melleor

Watu watano wameuawa baada ya washambuliaji kuvamia kanisa moja Afrika Kusini wakati malumbano yanaendelea juu ya uongoz [ ... ]

RAIS MAGUFULI AMTEUA MAMA SAMIA KUWA MGOMBEA MWENZA.
11 Jul 2020 16:21 - Grace Melleor

Rais Magufuli amemchagua Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea mweza katika Uchaguzi wa Urais wa Tanzania, Oktoba 2020.

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.