Star Tv

Wafugaji na wakulima wadogo katika  kata ya Lugaba mkoani Shinyanga wamelalamikia tabia ya wafanyabishara wa maziwa mkoani humo kuwakosesha soko la uhakika  kutokana na kuongeza maji katika kimiminika hicho na kupelekea idadi kubwa ya watumiaji kupungua kununua maziwa kwa madai ya kutokuwa na ubora.

Hayo yamebainishwa na wafugaji wa kata ya Lubaga ambao ni wananchama wa mtandao wa vikundi vya wakulima wadogo nchini MVIWATA  wakati wakikabidhiwa ngombe 20 wa maziwa na serikali ya mkoa wa shinyanga waliotolewa na mtandao wa wakulima MVIWATA kwa wafugaji katika kata hiyo.

Licha ya Kupata ng'ombe hao wa maziwa, wafugaji hao wamesemas wana wasiwasi juu ya soko la uhakika wa bidhaa hiyo kutokana na watumiaji kulalamika kuuziwa maziwa yasiyokuwa na ubora unaotakiwa.

Uongozi wa kata hiyo ukiongozwa na  diwani pamoja na afisa mifugo wanakili uwepo wa changamoto hiyo ya soko la maziwa.

Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Mkuu wa Wilaya ya shinyanga Yasinta Mboneko amekemea kitendo hicho cha wafanyabishara kuongeza maji katika maziwa.

Aidha ukosefu wa malisho pamoja na kiwanda cha kusindika maziwa kwa wafugaji hao vimetajwa  navyo kama bado changamoto zinazowakabili.

Ngombe hao  20 wenye thamani ya Shilingi milioni 30 wamenunuliwa kwa wafugaji mkoani Arusha na mtandao huo wa wakulima MVIWATA ikiwa ni sehemu mojawapo ya kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya kuwakwamua wananchi wake kiuchumi.

 

                                                                                                                         Mwisho

 

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.