Star Tv

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party TLP Augustino Mrema ameitaka Serikali kumlipa Shilingi bilioni mbili kama fidia ya kesi alizowahi kushtakiwa chini ya serikali ya awamu ya tatu iliyokuwa inaongozwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Mrema ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini dar es salaam wakati akizungumzia hali ya kisiasa nchini katika kipindi cha miaka 24 iliyopita hadi sasa.

Mwenyekiti huyo wa TLP amesema kutokana na misukosuko aliyoipata kwa kufunguliwa kesi za mara kwa mara, Serikali inapaswa kumlipa fidia ya kiasi hicho cha fedha.

 “Ninataka serikali ya CCM ambayo ndio imenufaika na mateso niliyopata kwa miaka yote wanifidie shilingi bilioni 2, hela ndogo ya chumvi na wasiponifidia nitawashtaki kwa watanzania.” Amesema Augustino Mrema-Mwenyekiti wa TLP Taifa.

Katika hatua nyingine Mrema amesema hakufurahishwa na vitendo vilivyofanywa katika uchaguzi wa serikali za mitaa hasa katika kijiji cha Kiraracha wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro akieleza kuwa zilikuwa ni hujuma za wazi dhidi yake.

Mbali na fidia, pia Mrema aliyepata kugombea nafasi ya Urais na kuleta upinzani mkubwa katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995 amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli iliyo na malalamiko na kuomba kukutana naye ili waweze kuzungumza.

                                                                                                       Mwisho.

 

Latest News

ZANZIBAR YAFUNGUA MILANGO KWENYE UTALII.
06 Jun 2020 10:30 - Grace Melleor

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeruhusu kuanzia leo safari za ndege za kitalii kuwasili nchini baada ya mambukizi ya [ ... ]

UFARANSA YATANGAZA KIFO CHA KIONGOZI WA AL-QAEDA.
06 Jun 2020 08:27 - Grace Melleor

Waziri wa Jeshi wa Ufaransa Florence Parly ametangaza kifo cha kiongozi wa al-Qaeda katika ukanda wa Maghreb (Aqmi) Abde [ ... ]

MZOZO WA SERIKALI YA LIBYA NA HAFTARI WAENDELEA KUSHIKA KASI.
06 Jun 2020 07:20 - Grace Melleor

Serikali ya Libya yadai kuuteka mji muhimu kutoka kwa hasimu wake Khalifa Haftar.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.