Star Tv

Watu 73 walifariki jana nchini China bara kutokana na homa ya virusi vya corona, na kufikisha idadi ya vifo vya maradhi hayo kufika 563.

Zaidi ya asilimia 80 ya vifo na maambukizi nchini China vinatokea katika mkoa wa Hubei ilikoanzia homa hiyo hatari. Hadi wakati huu watu wawili wameuawa na maradhi ya hayo nje ya China Bara, mmoja nchini Ufilipino na mwingine katika kisiwa cha Hong Kong, na wahanga wote hao walikuwa wameutembelea mji wa Wuhan ambao ni chimbuko la ugonjwa huo.

Kitisho cha ugonjwa huo kinaripotiwa kuongezeka katika meli ya anasa ya kijapani iliyozuiliwa katika bandari ya Yokohama, ambapo wizara ya afya ya Japan inasema watu 20 kati ya 3,700 waliomo ndani ya meli hiyo iliyowekwa katika karantini, wamethibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

                                                                                    Mwisho.

Latest News

WAKRISTO KUJITAFARI NA KWARESMA.
26 Feb 2020 17:45 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania TEC Padre Dokta Charles Kitima amesema kipindi cha kwaresima ni fursa ya kuji [ ... ]

CORONA YAENDELEA KUONGEZA IDADI YA VIFO IRAN.
26 Feb 2020 10:58 - Grace Melleor

Watu wawili walioambukizwa virusi vya Corona nchini Iran wamefariki, na kufikisha idadi ya waliofariki nchini humo kuwa  [ ... ]

BURIANI RAIS HOSNI MUBARAK.
26 Feb 2020 10:00 - Grace Melleor

Aliyekuwa rais wa zamani nchini Misri ambaye alitawala taifa hilo kwa miaka 30 Hosni Mubarak amefariki dunia hapo jana F [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.