Star Tv

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mghwira ameuagiza uongozi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA kuchukua hatua za dharura ili kuimarisha hali ya usalama  uwanjani hapo kwa kuongeza mitambo ya kubaini watu wenye vimelea vya

Taarifa na Zephania Renatus

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mghwira ametoa kauli hiyo alipotembelea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA  akiongozana na kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa  kwa lengo la kuangalia hatua zinazochukuliwa uwanjani  hapo katika kukabili Magonjwa ya mlipuko .

Kauli hiyo imefuatiwa na taarifa zilizodokeza  kuwa ,uwanja huo una mtambo mmoja tu wa kubaini endapo mgeni yoyote ataingia nchini akiwa na dalili za magonjwa  ya mlipuko  ikiwemo  virusi vya corona vinavyotajwa kuendelea kuua mamia ya raia wa china..

Pamoja na hayo,Mkurugenzi mtendaji katika Uwanja wa KIA Mhandisi Christopher Mukoma amesema idara ya kitengo cha afya  bado inakabiliwa na upungufu wa watumishi.

Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA  umekuwa ni lango la kuingia na kutoka ,na zaidi ya wageni elfu mbili kutoka mataifa mbalimbali wamekuwa wakiingia na kutoka kwa kila siku kupitia lango hilo.

                                                                             Mwisho

Latest News

WAKRISTO KUJITAFARI NA KWARESMA.
26 Feb 2020 17:45 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania TEC Padre Dokta Charles Kitima amesema kipindi cha kwaresima ni fursa ya kuji [ ... ]

CORONA YAENDELEA KUONGEZA IDADI YA VIFO IRAN.
26 Feb 2020 10:58 - Grace Melleor

Watu wawili walioambukizwa virusi vya Corona nchini Iran wamefariki, na kufikisha idadi ya waliofariki nchini humo kuwa  [ ... ]

BURIANI RAIS HOSNI MUBARAK.
26 Feb 2020 10:00 - Grace Melleor

Aliyekuwa rais wa zamani nchini Misri ambaye alitawala taifa hilo kwa miaka 30 Hosni Mubarak amefariki dunia hapo jana F [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.