Star Tv

Aliyekuwa rais wa zamani nchini Misri ambaye alitawala taifa hilo kwa miaka 30 Hosni Mubarak amefariki dunia hapo jana Februari 25, 2020 akiwa na umri wa miaka 91.

Kifo cha Hosni Mubarak kilithibitishwa na familia yake pamoja na televisheni ya taifa na Gazeti la Al-Ahram mjini Cairo,Misri.

Viongozi mbali mbali wa dunia wametoa salamu zao za rambirambi, wakisifu mchango alioutoa katika kusimamia uthabiti katika eneo la Mashariki ya Kati.

Mubarak aliitawala Misri kwa miaka 30, hadi pale alipoondolewa madarakani kufuatia maandamano makubwa ya umma mnamo mwaka 2011.

Jumamosi mwanae wa kiume Alaa Mubarak aliandika kwenye mtandao wake wa twitter kwamba baba yake ni mgonjwa na anapewa amepewa huduma ya matibabu ya wagonjwa mahututi, ambapo alisema kwamba baba yake alifanyiwa upasuaji mwezi Januari lakini hakutoa ufafanuzi zaidi.

Miongoni mwa maoni ya mwanzo kutolewa baada ya kutangazwa kifo chake ni pamoja na rais wa sasa wa Misri,ambae ikulu ilituma rambirambi za pole kwa familia ya Mubarak, ilimuelezea kuwa miongoni mwa ''mashujaa wa vita vya oktoba 73'' dhidi ya Israel,ambavyo  Hosni Mubarak aliongoza kikosi cha jeshi la anga.

Rais wa mamlaka ya wa palestina, Mahmoud Abbas alimuita rais huyo wa zamani wa Misri kuwa mtu aliepigania haki za wapalestina.

Kwa upande wake waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alipongeza ukakamavu wa Mubarak kwa ajili ya amani na usalama wa watu wake na kukamilisha amani na Israel.

Ayman Nouur ambaye ni mpinzani wa mda mrefu nchini Misri na mgombea wa uchaguzi wa mwaka 2012,anayeishi uhamishoni nchini Uturuki alituma rambirambi zake za pole kwa mtandao wake wa twita huku akisema ''amemsamehe kibinafsi'' Hosni Mubarak.

Hosni Mubarak alikamatwa mwezi Aprili, 2011 ikiwa ni miezi miwili tangu alipoondolewa mamlakani na baadae kupatiwa matibabu kwenye hospitali za magereza na kijeshi hadi mwaka 2017, wakati alipoachiwa baada ya kuondolewa mashitaka yaliyokuwa yakimkabili ya kuamuru mauaji dhidi ya waandamanaji.

Alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha jela mnamo mwaka 2012 kwa madai ya kula njama ya mauaji ya waandamanaji 239, lakini mahakama ya rufaa iliamuru kesi hiyo kusikilizwa upya na hatimaye mashitaka yake yalifutwa na aliachiliwa mwaka 2017.

Wamisri wengi walioishi enzi ya utawala wa Mubarak wanachuhukulia wakati huo kama kipindi cha utawala wa kiimla na ubepari na kuondolewa kwake madarakani kulifungua njia kwa Misri kufanya uchaguzi huru na wa kwanza uliomwingiza madarakani rais kutoka vuguvugu la Kiislamu, Mohamed Mursi.

Katika enzi ya uhai wake, Mubarak alisema hakufanya kosa lolote na kwamba historia itamuhukumu yeye kama mzalendo aliyehudumia taifa lake bila ya kuwa mbinafsi.

Hosni Mubarak anatazamiwa kuzikwa leo Jumatano Februari 26, 2020  kwa heshma za kijeshi.

 Mwisho.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.