Star Tv

Watu wawili walioambukizwa virusi vya Corona nchini Iran wamefariki, na kufikisha idadi ya waliofariki nchini humo kuwa watu 16.

Maafisa kutoka wizara ya afya nchini humo wametoa taarifa hizo leo wakati Wairan wakiwa na hofu kuwa huenda viongozi hawatilii maanani kiwango cha maambukizi.

Iran ina idadi kubwa ya vifo kutokana na virusi vya Corona nje ya China, ambako virusi hivyo vilianzia mwishoni mwa mwaka 2019.

Miongoni mwa wale walioambukizwa ni pamoja na Naibu Waziri wa afya, ambaye alipatikana kuwa ameambukizwa virusi hivyo vya Corona.

Maambukizi mapya ya virusi vya Corona vimethibitishwa leo nchini Italia pamoja na Austria, Croatia na nchini Uhispania, masaa kadhaa kabla ya mkutano wa mawaziri wa afya wa Umoja wa Ulaya unaofanyika leo.

Waziri mkuu wa Croatia Andrej Plenkovic amesema nchi hiyo ina mgonjwa mmoja huku jumla ya idadi  ya wagonjwa nchini Italia imepanda hadi  kufikia watu 283, ikiwa ni ongezeko la watu 54.

                                                    Mwisho.

Latest News

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AAMURU MASHAMBULIO DHIDI YA MJI WA MEKELLE.
26 Nov 2020 14:38 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema ameanzisha "awamu ya mwisho" ya operesheni ya kijeshi katika jimbo la Tigray  [ ... ]

WAZIRI MKUU MSTAAFU WA SUDAN AFARIKI KWA CORONA.
26 Nov 2020 14:25 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa zamani wa Sudan, Sadiq al-Mahdi amefariki dunia kutokana na virusi vya corona.

UAE YASITISHA UTOAJI VIZA KWA WAKENYA NA MATAIFA MENGINE 12 YA KIISLAMU.
26 Nov 2020 13:15 - Grace Melleor

Umoja wa Falme za Kiarabu, (UAE) umesitisha utoaji viza kwa Wakenya na mataifa mengine 12 ya Kiislamu

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.