Star Tv

Mahakama ya Israel leo Machi 10, 2020 imekataa ombi la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu la kutaka kufungua kesi ya rushwa dhidi yake anbayo imeahirishwa  hadi wiki ijayo.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Machi 17,2020 ambapo kwasasa imekuja wakati Netanyahu na washirika wake wa wakijaribu kuunda serikali huku wakikabiliwa na upinzani mkali kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita.

Wabunge walioko upande wa Netanyahu ambaye ni Waziri Mkuu wa kwanza kushtakiwa akiwa madarakani, wameiambia mahakama hiyo ya wilaya mjini Jerusalem kwamba hawakupokea nyaraka zote za upande wa mwendesha mashtaka kuhusu kesi hiyo na wametaka wapewe muda wa siku 45.

Netanyahu anashtakiwa kwa tuhuma za udanganyifu, suala la rushwa na utumiaji mbaya wa madaraka pia akidaiwa kupokea zawadi kama takrima kinyume cha sheria ambapo kwa upande wake Waziri mkuu Netanyahu amekanusha madai hayo.

                          Mwisho.

 

Latest News

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AAMURU MASHAMBULIO DHIDI YA MJI WA MEKELLE.
26 Nov 2020 14:38 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema ameanzisha "awamu ya mwisho" ya operesheni ya kijeshi katika jimbo la Tigray  [ ... ]

WAZIRI MKUU MSTAAFU WA SUDAN AFARIKI KWA CORONA.
26 Nov 2020 14:25 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa zamani wa Sudan, Sadiq al-Mahdi amefariki dunia kutokana na virusi vya corona.

UAE YASITISHA UTOAJI VIZA KWA WAKENYA NA MATAIFA MENGINE 12 YA KIISLAMU.
26 Nov 2020 13:15 - Grace Melleor

Umoja wa Falme za Kiarabu, (UAE) umesitisha utoaji viza kwa Wakenya na mataifa mengine 12 ya Kiislamu

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.