Star Tv

Serikali ya Rwanda imethibitisha visa vingine vinne vya maambukizi ya Corona na kufikisha idadi ya watu walioambukizwa kufikia watano, hali ambayo inawatia hofu raia wa Rwanda.

Wagonjwa wote waliwasili nchini Rwanda kutoka mataifa yaliyoathiriwa wakati huu serikali ya nchi hiyo ikitangaza hatua zaidi dhidi ya maambukizi hayo ambayo sasa yamefika katika eneo la Afrika Mashariki.

Rwanda ilithibitisha kisa chake cha kwanza cha virusi vya Corona (COVID-19) Jumamosi ya wiki hii iliyopita. Mgonjwa huyo ni raia wa India aliyewasili Rwanda Machi 8 kutoka Mumbai, India, kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara ya afya.

Raia huyo hakuwa na dalili zozote za virusi vya Corona wakati aliwasili nchini Rwanda na alijipeleka mwenyewe kwenye kituo cha afya Machi 13, ambapo alifanyiwa vipimo mara moja.

Hata hivyo kupitia mahojiano na kituo cha redio cha taifa cha Radio Rwanda, Waziri wa Afya wa Rwanda Dkt Ngamije Daniel, alisema kwamba nchi yake iko tayari kupambana na virusi hivyo.

Kupitia ujumbe wake katika mtandao wa Twitter, Rais Paul Kagame amewatakia wagonjwa wote afueni ya haraka na kumshukuru Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkuu wa Shirika la Afya Duniani la Umoja wa Mataifa (WHO), na idara yote kwa ujumla kwa uongozi wao wakati huu wa majaribu na kuwaombea wahudumu wa afya kuendelea kuwa imara wanapokuwa mstari wa mbele kukabiliana na janga hili.

Raia wa Rwanda wametakiwa kutohudhuria mikusanyiko ya umma na kuarifu mamlaka iwapo watashuhudia tukio wanalolishuku kupiga simu kupitia nambari 114.

Wakati huo huo shirika la ndege la Rwanda, Rwandair, limetangaza kusitisha safari zake za ndege kwa muda kwenda nchini India kwa sababu ya mlipuko wa Corona hadi Aprili 30, 2020.

        Mwisho.

Latest News

KENYA KUTUMA NDEGE CHINA KUCHUKUA VIFAA VYA COVID-19.
06 Apr 2020 15:17 - Grace Melleor

Waziri wa Usafirishaji wa Kenya James Macharia amesema wanatarajia kutuma ndege ya Kenya Airways nchini China siku ya Ju [ ... ]

WAGONJWA WAPYA WANNE WABAINIKA KUWA NA MAAMBUKIZI NCHINI.
06 Apr 2020 14:55 - Grace Melleor

Waziri wa afya Ummy Mwalimu ametoa taarifa ya uwepo wa ongezeko la wagonjwa wanne wa Corona ambapo watu hao wamepatikana [ ... ]

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA ALAZWA HOSPITALI MJINI LONDON.
06 Apr 2020 06:26 - Grace Melleor

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ya Downing Streeet imeeleza kuwa Waziri huyo amelazwa hospitalini ili ku [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.