Star Tv

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ametangaza ongezeko la visa viwili vya wagonjwa wenye maambukizi ya virusi vya corona.

Watu hao waliogundulika na virusi vya ugonjwa huo ni raia wawili wakigeni, mmoja amepatikana akiwa Zanzibar ambaye ni raia wa Ujerumani na mwingine yupo Dar es Salaam ambaye ni raia kutoka nchini Marekani.

Waziri wa afya Ummy Mwalimu siku ya Jumatatu Machi 16, 2020 alitangaza  kuwepo kwa kisa cha kwanza cha mtu mwenye maambukizi ya mgonjwa mmoja mwenye maambukizi ya virusi vya Corona ambaye ni mwanamke na  alikuwa ni Mtanzania.

Mpaka kufikia siku ya Jumanne Machi 17, 2020 Waziri Mkuu Majaliwa alitangaza kufunga shule zote (za awali, msingi na sekondari) kwa siku 30 na leo asubuhi Machi 18, 2020 Waziri Mkuu ametangaza vyuo vikuu vya elimu ya kati na vyuo vikuu kusitisha masomo ikiwa ni hatua ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya corona nchini humo.

Ameitaka wizara ya elimu kuafanya marekebisho ya ratiba ya mitihani ya kidato cha sita ambao walitarajiwa kufanya mitihani tarehe 4 Mei, itasogezwa mbele kadiri ya matokeo yatakavyojitokeza ili nao wapate kusoma kwa kipindi kilekile kilichokubalika na ratiba hiyo.

Michezo yote inayokusanya makundi ya watu kama vile ligi kuu ya Tanzania, Ligi daraja la pili, ligi daraja la kwanza lakini pia michezo ya shule za msingi (UMITASHUMTA) , michezo ya shule za sekondari(UMISETA) pamoja na michezo ya mashirika ya umma imetangazwa kusitishwa na Waziri  Mkuu kuanzia jana.

Waziri Mkuu Majaliwa amesma kuwa nchi imejiandaa vyema kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa huu wa Corona.

                          Mwisho.

 

Latest News

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AAMURU MASHAMBULIO DHIDI YA MJI WA MEKELLE.
26 Nov 2020 14:38 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema ameanzisha "awamu ya mwisho" ya operesheni ya kijeshi katika jimbo la Tigray  [ ... ]

WAZIRI MKUU MSTAAFU WA SUDAN AFARIKI KWA CORONA.
26 Nov 2020 14:25 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa zamani wa Sudan, Sadiq al-Mahdi amefariki dunia kutokana na virusi vya corona.

UAE YASITISHA UTOAJI VIZA KWA WAKENYA NA MATAIFA MENGINE 12 YA KIISLAMU.
26 Nov 2020 13:15 - Grace Melleor

Umoja wa Falme za Kiarabu, (UAE) umesitisha utoaji viza kwa Wakenya na mataifa mengine 12 ya Kiislamu

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.