Star Tv

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuweka mara moja marufuku ya kusafiri kwa raia wa kigeni wanaoingia Ulaya kwa muda wa siku 30 ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel amesema viongozi hao wameelezea umuhimu wa kushirikiana kufanya kila linalowezakana kukabiliana na janga hilo pamoja na athari zake na wamekubaliana kuweka vizuizi vya mpakani haraka iwezekanavyo.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema nchi yake itaanza kuweka marufuku ya kusafiri kwa raia wasio wa Ulaya haraka iwezekanavyo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas ameiambia DW kuwa operesheni ya kuwaondoa raia wa Ujerumani waliokwama nje ya nchi imeanza.

Wakuu wa mataifa yenye nguvu kiuchumi, G20 wanatarajia kukutana wiki ijayo kuzungumzia jinsi ya kukabiliana na janga la virusi vya corona.

Uingereza imetenga Pauni bilioni 330 za mkopo, ili kuzisaidia biashara zilizoathirika kutokana na virusi hivyo.

                             Mwisho.

Latest News

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AAMURU MASHAMBULIO DHIDI YA MJI WA MEKELLE.
26 Nov 2020 14:38 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema ameanzisha "awamu ya mwisho" ya operesheni ya kijeshi katika jimbo la Tigray  [ ... ]

WAZIRI MKUU MSTAAFU WA SUDAN AFARIKI KWA CORONA.
26 Nov 2020 14:25 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa zamani wa Sudan, Sadiq al-Mahdi amefariki dunia kutokana na virusi vya corona.

UAE YASITISHA UTOAJI VIZA KWA WAKENYA NA MATAIFA MENGINE 12 YA KIISLAMU.
26 Nov 2020 13:15 - Grace Melleor

Umoja wa Falme za Kiarabu, (UAE) umesitisha utoaji viza kwa Wakenya na mataifa mengine 12 ya Kiislamu

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.