Star Tv

Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amelitaka shirika la viwango nchini TBS na tume ya ushindani FCC kuacha kukaa ofisini badala yake wachunguze bei na uzalishwaji wa bidhaa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona ili ziweze kupatikana kwa urahisi na kwa bei elekezi.

Tamko hili limekuja siku chache mara baada ya serikali kupitia wizara ya afya kuthibitisha uwepo wa virusi vya corona nchini, upatikanaji wa bidhaa za usafi wa mikono yaani sanitizer, barakoa na vitakasa mikono pamoja na kemikali za usafi wa mazingira katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam umekuwa na changamoto kutokana na kupanda kwa bei,

Mbali na changamoto hiyo lakini bado kiwango halisi kinachohitajika katika vitakasa mikono hivyo kimekua na sintofaghamu pamoja na bei elekezi inayopaswa kufuatwa na wauzaji wa bidhaa hizo.

Waziri Bashungwa baada ya kusikia hayo akatumia nafasi hiyo kutembelea baadhi ya viwanda vinavyofanya uzalishaji wa bidhaa za vitakasa mikono kuangalia namna ambayo serikali inaweza kuwaongezea uwezo ili kuzalisha bidhaa hizo kwa wingi na kukidhi mahitaji yaliyopo sasa.

Mbali na kutembelea viwanda hivyo, imedhihirika kuwa viwanda vilivyopo sasa nchini  vina uwezo wa kuzalisha vitakasa mikono lita 5000 kwa siku huku huitaji ukiwa ni lita laki tatu na elfu hamsini.

Serikali imesema haitasita kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwanyang’anya leseni wafanyabiashara ambao watabainika wanatumia mlipuko wa virusi vya corona kama sehemu ya kujipatia faida kubwa.

                                                                  Mwisho.

 

 

Latest News

KENYA KUTUMA NDEGE CHINA KUCHUKUA VIFAA VYA COVID-19.
06 Apr 2020 15:17 - Grace Melleor

Waziri wa Usafirishaji wa Kenya James Macharia amesema wanatarajia kutuma ndege ya Kenya Airways nchini China siku ya Ju [ ... ]

WAGONJWA WAPYA WANNE WABAINIKA KUWA NA MAAMBUKIZI NCHINI.
06 Apr 2020 14:55 - Grace Melleor

Waziri wa afya Ummy Mwalimu ametoa taarifa ya uwepo wa ongezeko la wagonjwa wanne wa Corona ambapo watu hao wamepatikana [ ... ]

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA ALAZWA HOSPITALI MJINI LONDON.
06 Apr 2020 06:26 - Grace Melleor

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ya Downing Streeet imeeleza kuwa Waziri huyo amelazwa hospitalini ili ku [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.