Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema mpaka watu idadi a wagonjwa wa virusi vya Corona wamefikia 12.

Wagonjwa nane katika wagonjwa hao 12 waliotajwa na Rais Magufuli leo Machi 22, 2020 walioripotiwa leo na wengine wanne ni raia wa kigeni.

Rais Magufuli amesema kuwa Watanzania  waache kuwa na wasiwasi mpaka kufika mahali watu wanamsahau Mwenyezi  Mungu ndiye mponyaji wa kweli katika maisha ya kila siku kwa watu wote .

Mbali na kuwahusia wananchi kuafanya kazi kwa bidi na  kuacha kupeana  hofu kupitia mitandao ya kijamii na badala yake kuzingatia taarifa za kweli kutoka mamlaka husika.

Taarifa zinaeleza kuwa wakati virusi vya ugonjwa huu ulipoanza kusambaa Shirika la Afya Duniani (WHO) liliutangaza ugonjwa wa Covid-19 kuwa wa Dharura ya Kimataifa.Hata hivyo, kutokana na kasi ya kusambaa kwake Machi 11, 2020, WHO limeutangaza ugonjwa huu kuwa Janga la Kimataifa.

Katika juhudi za kudhibiti kuenea kwa maaambukizi Rais Magufuli amesema kuanzia Jumatatu, wageni wote watakaoingia nchini kutoka mataifa yaliyoriupotiwa kuwa na visa vya ugonjwa huo watatengwa kwa siku 14 kwa gharama zao.

Jumanne wiki hii Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitangaza kufunga shule pamoja na vyuo vyote kwa siku 30 ikiwa ni hatua ya kuzuia kuenea kwa maambukizi mapya  ya Virusi vya corona nchini .

Mbali na kufunga shule na vyuo serikali imezuia mikusanyiko yote ya watu wengi yakiwemo matamasha ya muziki, mikutano ya hadhara mbalimbali ikiwemo ya kisiasa pamoja na michezo.

                Mwisho.

Latest News

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AAMURU MASHAMBULIO DHIDI YA MJI WA MEKELLE.
26 Nov 2020 14:38 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema ameanzisha "awamu ya mwisho" ya operesheni ya kijeshi katika jimbo la Tigray  [ ... ]

WAZIRI MKUU MSTAAFU WA SUDAN AFARIKI KWA CORONA.
26 Nov 2020 14:25 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa zamani wa Sudan, Sadiq al-Mahdi amefariki dunia kutokana na virusi vya corona.

UAE YASITISHA UTOAJI VIZA KWA WAKENYA NA MATAIFA MENGINE 12 YA KIISLAMU.
26 Nov 2020 13:15 - Grace Melleor

Umoja wa Falme za Kiarabu, (UAE) umesitisha utoaji viza kwa Wakenya na mataifa mengine 12 ya Kiislamu

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.