Star Tv

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amethibitisha kutokea kwa vurugu za wagonjwa waliowekwa katika uangalizi ambao walikutwa na maambukizi ya corona katika Hospitali ya Amana wakitaka kutoroka hospitalini hapo na kurejea nyumbani.

Leo asubuhi katika mitandao ya kijamii, ilisambaa sauti ikielezea wagonjwa katika Hospitali ya Amana wenye maambukizi ya virusi vya corona kutoroka na wengine kupanda daladala hali iliyozua hofu katika jamii.

Wagonjwa hao wanadaiwa kutoroka hospitalini hapo leo Alhamisi Aprili 23, wakidai kuna msongamano wa wagonjwa wengi huku kukiwa hakuna dawa wala chakula na wao wanaendelea vizuri lakini hawaruhusiwi kurejea nyumbani.

Akitoa ufafanuzi wakati akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, Bi. Mjema amesema si kwamba wametoroka ila wagonjwa hao wamechoka kukaa ndani ya kituo hicho cha uangalizi na hawataki kuendelea kukaa hospitalini hapo.

Bi Mjema amesema kuwa;“Kuna wagonjwa walikuwa wamefika pale wakasema wao hawaumwi sana kwa hiyo walikuwa wanataka waruhusiwe, sasa ukifika pale kama una dalili za maambukizi ya corona lazima ukae kwanza uangaliwe, sasa wao hawataki wanataka waruhusiwe walikuwa wanapiga kelele wanataka kuondoka".

Amesema kuwa endapo mtu ana viashiria au dalili za corona, na ana wasiwasi wa kujiona si mzima, anapaswa kuchukua tahadhari haraka na amewashauri watu kuacha kuamini mambo yanayosemekana mtaani bali wasikilize serikali pamoja na wataalamu wa afya wanachosema, Pia waache kufanya vurugu kwani kufanya hivyo haisaidii kumaliza janga hili la ugonjwa wa Corona.

Latest News

MPAKA WA HOLILI NA NAMANGA BADO KIZUNGUMKUTI.
05 Jun 2020 14:06 - Grace Melleor

Mipaka miwili ya Tanzania na Kenya eneo la Namanga na Holili imefungwa tena baada ya kuibuka hali ya sintofahamu kuhusu  [ ... ]

CWT YAZUNGUMZA UKWELI WA MSHAHARA WANAOLIPWA.
05 Jun 2020 10:23 - Grace Melleor
Notice: Undefined property: stdClass::$thumb in /var/www/html/startv.co.tz/public_html/startvweb/modules/mod_minifrontpage/themes/default/tmpl/bottom.php on line 79

Chama cha Walimu Tanzania kimesema kinatambua jitihada kubwa ambazo zinafanywa na Serikali katika kuboresha maisha ya wa [ ... ]

RAIS TRUMP ASHUTUMIWA KUWAGAWANYA RAIA WAKE.
04 Jun 2020 10:28 - Grace Melleor

Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis amemshutumu Rais Donald Trump, kwa kuleta mgawanyiko na kutumia viba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.