Star Tv

Mahakama nchini Kenya imemuachilia huru mshukiwa wa mauaji Philip Onyancha kutokana na kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha.

Onyancha alikuwa anakabiliwa na kesi juu ya mauaji ya wanawake wawili Catherine Chelangat na Jackline Chepngetich mwaka 2008.

Katika uamuzi wake, Jaji Jessie Lesiit amesema waendesha mashitaka katika kesi hiyo hawakutoa ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani mshukiwa.

Jaji alisema uchunguzi juu ya kesi hiyo ulitaka na ulikuwa "mapungufu ya kuvunja moyo"

Bw. Onyancha, ambaye alikana makosa mashitaka mwaka 2014 mahakamani alidai kuwa hakutekeleza uhalifu.

Mshukiwa alikana mashitaka baada ya kufanyiwa vipimo vya kiakilina ripoti kuonyesha kwamba ana uwezo wa kukiri au kukana mashitaka , kufuatilia kesi, na kumpa maagizo wakili wake.

Awali Onyancha, ambaye aliwaambia polisi na vyombo vya habari kwamba alihusika na mauaji, pia alikana kumuua Catherine Chelagat tarehe 22 Novemba 2008.

Taarifa ya hukumu juu ya kuachiliwa kwa Onyancha ilishirikishwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Kenya.

Aidha, pamoja na washitakiwa wenzake Tobias Nyabuhanga Aradi na Douglas Obiero Makori, alikana kumuua mvulana mwenye umri wa miaka 14 Anthony Njirwa Muiruri Aprili 14, 2014 katika kijiji cha Ngando Dagoretti, Nairobi.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

ALGERIA YATANGAZA SIKU 3 ZA KUOMBOLEZA KIFO CHA RAIS BOUTEFLIKA.
18 Sep 2021 18:38 - Grace Melleor

Kiongozi wa Algeria ametangaza siku tatu za maombolezo kuanzia leo hii, kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa taifa hilo,  [ ... ]

WAZIRI MKUU AAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE KATIKA UJENZI UNAOSUASUA.
18 Sep 2021 18:24 - Grace Melleor

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge kufuatilia kwa karibu ujenzi w [ ... ]

WAZIMBABWE AMBAO HAWAJACHANJWA WAZUIWA KUFANYA KAZI.
15 Sep 2021 14:18 - Grace Melleor

Zimbabwe imewazuia wafanyakazi wa umma ambao hawajanjwa kwenda kazini.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.