Star Tv

Rais wa zamani wa Mali Moussa Traoré amefariki dunia leo Jumanne Septemba 15,2020.

Chanzo kutoka familia yake kimeiambia Shirika la Habari la RFI Rais huyo wa zamani wa Mali amefariki ingawa hawakubainisha ugonjwa uliopeleka afariki.

Moussa Traoré, ambaye alizaliwa Septemba 25, 1936, alichukua hatamu ya uongozi wa nchi mwaka 1968 kabla ya kupinduliwa mwezi Machi 1991.

Rais Traoré alihukumiwa kifo, lakini mwaka 2020 Rais wa zamani Alpha Oumar Konaré alimsamehe.

Katika miaka ya hivi karibuni, Marehemu Traore amekuwa akisikilizwa sana miongoni mwa wanasiasa nchini Mali.

 

Latest News

HESLB YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA POTOFU INAYOSAMBAZWA MITANDAONI.
19 Oct 2020 17:32 - Grace Melleor

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imefafanua kuhusu taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusiana na utara [ ... ]

WAALIMU WAANZA MGOMO DR CONGO.
19 Oct 2020 17:02 - Grace Melleor

Nchini DRC, walimu kutoka chama cha walimu cha SYECO na wale kutoka chama cha walimu wa kikatolika (SYNECAT) wameanza mg [ ... ]

WANANCHI WA GUINEA WASUBIRI MATOKEO YA UCHAGUZI WA URAIS.
19 Oct 2020 16:25 - Grace Melleor

Baada ya miezi kadhaa ya maandamano mabaya dhidi ya muhula wa 3 wa rais Alpha Condé, wananchi wa Guinea walipiga kura k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.