Star Tv


Wafuasi wa Mhubiri wa Nigeria Temitope Balogun Joshua, maarufu kama TB Joshua wamekusanyinka katika makao makuu ya kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN) mjini Lagos kuomboleza kifo chake.

Kifo cha TB Joshua kilichotokea Jumapili Alfajiri kimeiibua maswali mengi huku baadhi ya watu wakitaka kujua kifo cha Nabii huyo kimesababishwa na nini.

Kanisa la SCOAN mpaka sasa halijathibitisha wala kusema chanzo cha kifo cha ghafla cha mhubiri huyo kimesababishwa na nini hasa.

Waumini wanaoishi karibu na kanisa hilo walikusanyika katika ukumbi wa kanisa baada ya kupokea taarifa za kifo ili kumuomboleza.

"Alikuwa mtu wa Mungu...sijawahi kuona mhubiri mkarimu anayewasaidia watu hata kama sio wafuasi wa kanisa lake," - Saidat ambaye ni muumini wa dini ya Kiislamu aliiambia BBC.

Nkiru, mmoja wa waombolezaji alisema "Nitamkosa sana.....sijui hili kanisa litaendele vipi baada ya kifo chake."

Mke wake Evelyn Joshua ambaye ni mmoja wa wahubiri wakuu wa kanisa la SCOAN alielezea kugutushwa na kifo cha ghafla cha muwe wake.

"Kumpoteza mwenza sio jambo rahisi; iwe ghafla au laaah, inavunja moyo, Majonzi huharibu ustawi wetu kwa ujumla. Lakini cha msingi ni kumtumainia Mungu”.-Alisema mke wa TB Joshua.

Aidha taarifa iliyotolewa na kanisa lake la SCOAN siku ya Jumapili alfajiri ilithibitisha TB Joshua amefariki akiwa na umri wa miaka 57.
#Chanzo:BBCSwahili

Latest News

NIGERIA YAPOKEA NDEGE SITA ZA KUPAMBANA NA WAASI.
23 Jul 2021 14:50 - Grace Melleor

Nigeria imepokea ndege sita za kijeshi iliyonunua kutoka Marekani, ambazo zinatarajiwa kupiga jeki juhudi za kukabiliana [ ... ]

WATU KADHAA WAKAMATWA KWA JARIBIO LA KUTAKA KUMUUA RAIS RAJOELINA.
22 Jul 2021 13:15 - Grace Melleor

Raia kadhaa wa mataifa ya kigeni pamoja na wengine wa nchini Madagascar wanashikiliwa na mamlaka nchini humo kwa tuhuma  [ ... ]

HABARI ZA HIVI PUNDE: ANNA MGHWIRA AFARIKI DUNIA.
22 Jul 2021 10:55 - Grace Melleor

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefariki dunia leo Julai 22, katika Hospitali ya Mount Meru.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.