Star Tv

Mwalimu mmoja wa shule ya msingi ya Gitega nchini Burundi yuko mikononi mwa polisi kwa shutuma za kuwatesa watoto wa shule anaowafundisha.

Mwalimu Espeye Nzeyimana Ecofo Ngobeke, ambaye ni mwalimu wa somo la Kifaransa darasa la nne anasemekana aliwaadhibu wanafunzi 30 kwa kushindwa kujibu maswali aliyowauliza.

Watoto 30 kati ya 45 ni wanafunzi wake waliofeli na akaamua kuwapa adhabu ya kuzunguka uwanja uliojaa mawe kwa magoti.

Magoti yao yalianza kuchubuka na kutokwa damu na ikabidi wapelekwe wote hospitalini kutibiwa.

Afisa elimu katika eneo la Mubuga ilipo shule ya Ngobeke Manirambona Placide, anasema mwalimu huyo yuko mikononi mwa polisi.

"Nzeyimana Esperee alisimamishwa kazi Jumapili asubuhi, na kupelekwa mjini Gitega ambako anasubiri kufikishwa mahakamani"- Alisema Bw. Manirambona Placide.

Taarifa zilizotolewa na polisi zinasema kuwa baada ya kuona jinsi wanafunzi wake walivyoumia, mwalimu huyo hakuonekana tena kazini.

ChanzoBBCSwahili

Latest News

NIGERIA YAPOKEA NDEGE SITA ZA KUPAMBANA NA WAASI.
23 Jul 2021 14:50 - Grace Melleor

Nigeria imepokea ndege sita za kijeshi iliyonunua kutoka Marekani, ambazo zinatarajiwa kupiga jeki juhudi za kukabiliana [ ... ]

WATU KADHAA WAKAMATWA KWA JARIBIO LA KUTAKA KUMUUA RAIS RAJOELINA.
22 Jul 2021 13:15 - Grace Melleor

Raia kadhaa wa mataifa ya kigeni pamoja na wengine wa nchini Madagascar wanashikiliwa na mamlaka nchini humo kwa tuhuma  [ ... ]

HABARI ZA HIVI PUNDE: ANNA MGHWIRA AFARIKI DUNIA.
22 Jul 2021 10:55 - Grace Melleor

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefariki dunia leo Julai 22, katika Hospitali ya Mount Meru.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.