Star Tv

Wanaume wawili wamejaribu kumdunga kisu Rais wa mpito wa Mali Assimi Goïta katika msikiti uliopo katika mji mkuu, Bamako.

KanaliGoïta allikuwa akihudhuria ibada ya siku ya Eid ul-Adha katika msikiti wa Grand Mosque.

Mafisa wanasema washambuliaji, ambao kwa mujibu wa Shirika la habari la AFP walikuwa ni wawili, wamekamatwa na rais ameondolewa kwenye msikiti huo kwa usalama wake.

Haijafahamika iwapo Kanali Goïta, ambaye aliongozajeshi kuchukua mamlaka mwezi Agosti, alijeruhiwa.

Waziri wa masuala ya kidini Mamadou Kone aliliambia shirika la AFP kwamba mwanaume ali "jaribu kumuua rais wa kisu".

Mkurugenzi wa msikiti aliliambia shirika la habari kwamba mtu alimlenga waziri lakini alimjeruhi mtu mwingine.

Kabla ya mapinduzi ya mwezi Agosti nchi hiyo ilikuwa inakabiliwa na maadamano juu ya ufisadi na waasi wa Kiislam walikuwa wameyateka maeneo mengi ya nchi.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

ALGERIA YATANGAZA SIKU 3 ZA KUOMBOLEZA KIFO CHA RAIS BOUTEFLIKA.
18 Sep 2021 18:38 - Grace Melleor

Kiongozi wa Algeria ametangaza siku tatu za maombolezo kuanzia leo hii, kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa taifa hilo,  [ ... ]

WAZIRI MKUU AAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE KATIKA UJENZI UNAOSUASUA.
18 Sep 2021 18:24 - Grace Melleor

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge kufuatilia kwa karibu ujenzi w [ ... ]

WAZIMBABWE AMBAO HAWAJACHANJWA WAZUIWA KUFANYA KAZI.
15 Sep 2021 14:18 - Grace Melleor

Zimbabwe imewazuia wafanyakazi wa umma ambao hawajanjwa kwenda kazini.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.