Star Tv

Tume ya uchaguzi nchini Misri imetangaza leo kwamba kura ya maoni kuhusu mageuzi ya katiba ikiwemo uwezekano wa kumruhusu rais Abdel-Fatah al sisi kubakia madarakani mpaka mwaka 2030,itafanyika Aprili 20-22.

Tangazo la tume hiyo limekuja baada ya hapo jana bunge la Misri kuidhinisha mageuzi ya katiba ambayo yatamruhusu rais el-Sisi kuendelea kujiimarisha madarakani. Maafisa wa Misri wanajaribu kuzuia kuongezeka kwa malalamiko yanayotolewa katika mtandao yakipinga mageuzi hayo. Bunge lenye wajumbe 596 linalohodhiwa na wafuasi wa el-Sisi lilihitaji wingi wa thuluthi mbili tu ya kura kupitisha mageuzi 14 na kuingiza vipengee vingine vingi vipya.

CHANZO:Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

Uhalifu Afrika Mashariki
19 Sep 2019 14:25 - Kisali Shombe

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa, amewataka wakuu wa polisi kutoka nchi kumi na nne zinazou [ ... ]

Watoto 26 wauawa katika ajali ya moto,Liberia.
19 Sep 2019 12:23 - Kisali Shombe

 Watoto 26 wamekufa katika ajali ya moto uliounguza shule moja ya Kiislamu karibu na mji mkuu wa Liberia, Monrovia.

Mamlaka ya Maji Maswa lawamani.
19 Sep 2019 12:11 - Kisali Shombe

Wakazi wa mji wa Maswa mkoani Simiyu wameilalamikia Mamlaka ya Maji na Usafi wa mazingira, (MAUWASA), kwa kitendo cha ku [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.