Star Tv

Kiongozi wa serikali ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa Fayez al-Sarraj ameapa kutorejea katika meza ya mazungumzo na kiongozi wa vikosi vya upinzani Khalifa Haftar kwa kuendeleza mashambulizi licha ya taifa hilo kuendelea kukabiliana na janga la Corona.

Wakati huo Serikali ya Libya inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa imewaachilia huru wanamgambo wa Jihadi waliokuwa wanazuiliwa katika miji miwili ya Magharibi nchini humo.


Kuachiliwa huru kwa wapiganaji hao kutoka makundi ya Jihadi waliokuwa wakisaidia serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya, kumezua wasiwasi miongoni mwa wakazi wa miji miwili ya Sorman na Sabratah.

Jumapili April 13,2020 majeshi ya serikali ya umoja wa kitaifa yalikamilisha operesheni ya kuyadhibiti maeneo ya pwani yote ya Magharibi hadi kwenye mpaka wa Tunisia, Maeneo ambayo hapo awali yalikuwa chini ya udhibiti wa vikosi vya Khalifa Haftar.


Libya inakumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo mbali na kuheshimu vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa mataifa, ambapo mzozo huo ni kati ya jenerali Khalifa Hiftar dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa GNA.

Mataifa ya kigeni katika mgogoro huu yanahusishwa haswa Uturuki ambayo inadaiwa kusaidia kwa kutoa silaha ili kuwezesha serikali ya Libya kuendelea na mapigano.

Jenerali Haftar wa kikosi cha wapiganaji anaungwa mkono na Urusi, Misri, Saudi Arabia, Jumuiya ya Mataifa ya kiarabu na Jordan.

Haftar ni afisa wa kijeshi wa zamani aliyemsaidia Kanali Muammar Gaddafi kuingia madarakani mwaka 1969 kabla ya kutofautiana na kiongozi huyo na hatimaye kukimbilia mafichoni nchini Marekani.

Alirejea nchini Libya mwaka 2011 baada ya maandamano ya kupinga utawala wa Gaddafi kuanza na kuwa Kamanda wa waasi.

Ghasia zimeikumba Libya tangu utawala wa kiongozi wa nchi hiyo wa muda mrefu, Muammar Gaddafi kuangushwa na yeye kuuawa mwaka 2011.

 

 

Latest News

MPAKA WA HOLILI NA NAMANGA BADO KIZUNGUMKUTI.
05 Jun 2020 14:06 - Grace Melleor

Mipaka miwili ya Tanzania na Kenya eneo la Namanga na Holili imefungwa tena baada ya kuibuka hali ya sintofahamu kuhusu  [ ... ]

CWT YAZUNGUMZA UKWELI WA MSHAHARA WANAOLIPWA.
05 Jun 2020 10:23 - Grace Melleor
Notice: Undefined property: stdClass::$thumb in /var/www/html/startv.co.tz/public_html/startvweb/modules/mod_minifrontpage/themes/default/tmpl/bottom.php on line 79

Chama cha Walimu Tanzania kimesema kinatambua jitihada kubwa ambazo zinafanywa na Serikali katika kuboresha maisha ya wa [ ... ]

RAIS TRUMP ASHUTUMIWA KUWAGAWANYA RAIA WAKE.
04 Jun 2020 10:28 - Grace Melleor

Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis amemshutumu Rais Donald Trump, kwa kuleta mgawanyiko na kutumia viba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.