Star Tv

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofanya kampeni za kuharibu jina la nchi hiyo.

Hatua hiyo ya tamko la Rais Mnangagwa imemulikwa na kukosolewa vikali na wanaharakati wa haki za binadamu.

Hii inakuja siku kadhaa baada ya Rais Emmerson Mnangagwa kuvishutumu vyama vya upinzani kwa kushirikiana na mabalozi wa nchi za Magharibi kuhujumu uchumi na kuchochea vitendo vya kigaidi.

Wakati huo huo shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch limezitolea mwito nchi za Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC, kukemea hadharani ukandamizaji uliofanywa na serikali ya Zimbabwe dhidi ya maandamano ya amani ya kupinga ufisadi yaliyofanyika Julai 31.

Shirika hilo pia limelaani kamatakamata ya kiholela dhidi ya wapinzani nchini humo.

Katika ripoti yake iliyochapishwa wiki hii, Human Rights Watch inasema kuwa serikali ya Zimbabwe imewakamata kuhusiana na maandamanano hayo, watu wasiopungua 60, ikiwa ni pamoja na mwandishi wa vitabu Tsitsi Dangarembga na msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha Movement for Democratic Change, MDC Fadzayi Mahere.

Baada ya ripoti hiyo ya Human Right Watch inayoorodhesha visa vya kuwakamata kinyume cha sheria wakosoaji wa serikali nchini Zimbabwe, wakiwemo mwandishi wa habari aliyetuzwa kwa kazi yake Hopewell Chin'ono, na kiongozi wa kundi la kisiasa linalotaka mabadiliko la Transform Zimbabwe, Jacob Ngarivhume Rais wa nchi hiyo akatoa tamko la kusema kuwa sheria itapitishwa ambayo itatoa adhabu kali kwa wanaochafua taifa hilo.

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.