Morocco imesema inatumia mbinu mpya katika kukabiliana na wimbi la wahamiaji wanaotaka kuitumia kama njia ya kuingilia Ulaya, na imefanikiwa kuwazuia wahamiaji 25,000 waliojaribu kuingia Uhispania kupitia njia ya Gibraltar kwa mwaka huu pekee.

Ingawa haikuelezea zaidi ni teknolojia gani wanayoitumia, lakini mkuu wa usalama wa mipakani wa Morocco, Khalid Zerouali, amesema kwenye mahojiano na shirika la habari la Associated Press kwamba teknolojia ya ufuatiliaji na vikosi imara kwa pamoja vimesaidia kuimarisha usimamizi. Zerouali amesema mafanikio hayo ni asilimia 30 zaidi, ikilinganishwa na mwaka jana ya kuwazuia wahamiaji kupitia Gibraltar kuingia Uhispania, na hususan kati ya miezi ya Februari na Aprili.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

Mauaji ya kukata makoromeo, washtakiwa wahukumiwa. Bukoba
20 Jun 2019 08:21 - Kisali Shombe

MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyo [ ... ]

Kudorola kwa soko la Pamba.
19 Jun 2019 12:20 - Kisali Shombe

Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhaki [ ... ]

Adha ya maji, Kalambo
19 Jun 2019 11:23 - Kisali Shombe

Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba   [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.