Star Tv

Raia nchini Ufaransa na Ujerumani wanapiga kura leo katika siku ya mwisho ya uchaguzi wa Bunge la Ulaya ambapo vyama vinavyopinga Umoja wa Ulaya pamoja na uhamiaji vinatumai kutoa changamoto kubwa.

Mbali ya Ujerumani na Ufaransa, ambayo ni mataifa yenye nguvu barani Ulaya, nchi nyingine karibu 20 wanachama wa Umoja huo zinapiga kura leo, ambayo ni siku ya mwisho ya uchaguzi huo wa Bunge la Ulaya. Zaidi ya wapiga kura milioni 400 wanashiriki uchaguzi huo katika mataifa 28 na matokeo rasmi yanatarajiwa baadaye leo jioni. Nchini Ujerumani, maoni ya umma ya kabla ya uchaguzi yalivipa nafasi ya ushindi wa asilimia 28 vyama ndugu vya kihafidhina vya CDU na CSU. Wanasiasa kutoka vyama vikuu nchini Ujerumani walitumia siku za mwisho kabla ya uchaguzi kutoa onyo dhidi ya kukipigia kura chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, AfD, kinachopinga wahamiaji na Umoja wa Ualya.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW.

Latest News

Vipimo vyabaini Mwandishi Kabendera anamatatizo katika pingili za mgongo.
18 Sep 2019 13:41 - Kisali Shombe

Mwandishi wa Habari za ,uchunguzi Erick Kabendera ├ámeielezea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa amepata huduma za Kit [ ... ]

Mhandisi wa Ujenzi wa wilaya ya Morogoro asimamishwa kazi.
18 Sep 2019 13:31 - Kisali Shombe

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhandisi wa Ujenzi wa wilaya ya Morogoro, Brown Undule baada ya kushindwa [ ... ]

Kukamatwa kwa Madini, Mara
18 Sep 2019 13:11 - Kisali Shombe

Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mara imekamata kilo tano za mchanga wenye madini ya dhahabu ukiwa na thamani ya s [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.