Kansela wa Austria Sebastian Kurz aliyeondolewa madarakani jana Jumatatu kupitia kura ya bunge ya kutokuwa na imani naye na hivyo kupisha njia kwa ajili ya uchaguzi mpya, ameapa kwamba chama chake kilicho na siasa za wastani za mrengo wa kulia kitarejea katika uongozi kikiwa na nguvu zaidi.

Kura hiyo dhidi ya kiongozi huyo kijana wa nchi na serikali au baraza lake la mawaziri ni ya kihistoria nchini Austria tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Kura hiyo imeungwa mkono na wabunge kutoka chama cha Social Democrats na chama cha Freedom kinachofuata siasa kali za mrengo wa kulia, ambacho kilikuwa katika serikali ya muungano ya Kurz hadi wiki moja iliyopita ambapo kiongozi wake alijiuzulu kutokana na kashfa ya rushwa. Kwa mujibu wa katiba, Rais wa Austria, Alexander Van der Bellen sasa anapaswa kumteua kansela mpya ambaye ataunda serikali ambayo itaungwa na mkono na bunge hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika. Uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwezi Septemba.

 

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

TTB Kusimamia masoko ya Tumbaku.
15 Jun 2019 10:21 - Kisali Shombe

Bodi ya tumbaku nchini,TTB imetoa onyo kwa watendaji  wa makampuni ya ununuzi wa tumbaku wanaokwenda kinyume na sheria [ ... ]

Jeshi la Sudan lakiri vikosi vya usalama vilikiuka sheria
15 Jun 2019 10:11 - Kisali Shombe

Baraza la kijeshi linalotawala Sudan limekiri kwamba vikosi vya usalama vilikiuka sheria wakati wa kuwatawanya waandaman [ ... ]

Wizi wa umeme, Dar es Salaam
15 Jun 2019 09:59 - Kisali Shombe

Shirika la umeme nchini Tanesco Kanda ya Dar es salaam limefanya ukaguzi wa akaunti za luku eneo la Mchikichini wilaya y [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.